Mwalimu Abasi Hussein wa shule ya msingi
Mwabomba iliyopo tarafa ya Ngula wilayani Kwimba mkoani Mwanza anashikiliwa na
jeshi la polisi kwa tuhuma za kukutwa darasani akifanya mapenzi na mwanafunzi
wa kidato cha nne mwenye umri wa miaka 17.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed
Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo mkoani humo na kusema mpaka sasa
mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 27 anashikiliwa na jeshi la polisi muda
wowote upelelezi ukikamilika mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani kujibu
tuhuma hizo.
“Babu wa mwanafunzi alipoona
mjukuu wake amechelewa kurudi nyumbani alianza kufanya msako alikwenda kwenye
shule ya sekondari lakini hakumuona ikabidi aendelee kumtafuta mjukuu wake,
ilipofika kwenye muda wa saa sita na kitu alikwenda kwenye shule ya msingi ya
Mabomba katika moja ya darasa wakamkuta huyo mwanafunzi wa kike akifanya
mapenzi na mwalimu wa shule hiyo ya msingi ya Mwabomba” alisema RPC Msangi
Kamanda Msangi ametoa onyo kwa watu
wanaojihusisha na mapenzi na watoto chini ya miaka 17 na kusema huenda awe
amekubali mwenyewe hilo ni kosa la ubakaji hivyo amewataka kuacha na kusema
kufanya vitendo hivyo ni sawa na kuhitaji kwenda jela miaka 30.
Post a Comment
karibu kwa maoni