Jeshi
la Polisi Dodoma linawashikilia watu 11 kwa uchunguzi kutokana na mauji
ambapo August 8, 2017 majira ya saa 4:00 usiku katika kitongoji cha
Chang’ombe Wilaya ya Chamwino mtu mmoja mwanamke aliyefahamika kwa jina
la Mariam Saidi miaka 17 mkazi wa Kigoma aliuawa kwa kukatwa shingo na
kutenganishwa na kiwiliwili na kuchomwa moto.
Mwili
wa marehemu ulikutwa nyumbani kwa mganga wa jadi aitwaye Ashura Mkanga
mwenye miaka 33 na mkazi wa kitongoji cha Chang’ombe ambapo mazingira
ya tukio yanaonesha kuwa mganga huyo wa jadi asiye na kibali kuendesha
shughuli za tiba asili analaza wagonjwa nyumbani kwake, anafanya
matambiko, anapiga ramli chonganishi, anafanya tohara za watoto katika
nyumba yake pamoja na matambiko.
“Tukio
hili ni baya na halikubaliki hapa Dodoma na mahala popote, ni fedheha
kubwa sana kwa wananchi kuendelea kukumbatia imani za kishirikina
katika karne hii na Serikali imesogeza huduma za afya karibu na jamii
lakini bado wapo watu hawataki kwenda hospitali na kukubali kuuawa kwa
fedheha na waganga wachonganishi.” Alisema Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Dodoma Lazaro Mambosasa wakati akiongea na waandishi wa habari
Post a Comment
karibu kwa maoni