Na gharos riwa bunda 0768443315
BUNDA.
Idadi ya wazee wenye umri wa kuanzi miaka 60 na
kuendelea wanaoishi katika kata ya Kunzugu Halmashauri ya mji wa Bunda Mkoani
Mara, wanaopaswa kupatiwa huduma za afya Bure kwa mujibu wa sera ya serikali
bado haieleweki licha ya diwani wa kata hiyo bwana Pasaka Samwel kueleza
chanzo chetu cha habari siku kadhaa zilizopita kuwa atalifuatilia
kuhakikisha kuwa wazee hao wanajulikana
kwa majina na kiidadi na waanza kupatiwa huduma hiyo kama kawaida.
Siku kadhaa zilizopita diwani huyo Bwana Pasaka
aliahidi kuwa atapanga utaratibu wa kukutana na wananchi pamoja na watendaji wake ili kuweka
utaratibu wa kuwabaini wazee wenye umri wa kuanzia miaka 60 kwa lengo la
kuchukua taarifa zao muhimu na kuziwasilisha ofisi ya mkrugenzi wa halmashauri ya mji huo ili waweze kupata
vitambulisho vitakavyowawezesha kupata huduma ya afya bure, lakini hali
inaonekana kutoridhisha baada ya taratibu hizo kutozaa matunda na kupatikana taarifa za kumkatisha tamaa diwani huyo.
Akizungumza na chanzo chetu cha habari kwa njia ya
Simu bwana Pasaka amethibitisha kuwa hajapata jina la mzee hata
mmoja kutoka kwa watendaji wake,kitendo kilichomfanya kuwatupia lawama
wenyeviti wa vitongoji, wenyeviti wa vijiji pamoja na watendaji kushindwa
kuwabaini wazee hao kwakuwa wao ndio wako karibu nao zaidi.
Kuhusu kufanya mkutano katika vijiji vyote
vinavyounda kata hiyo diwani huyo amesema tayari walishakutana na kuweka
makubaliano kuwa taarifa zifikishwe kwa watendaji ili yeye kama diwani aweze
kuzipokea na kuzifikisha halmashauri lakini viongozi hao wameshindwa kufanya
kazi hiyo ipasavyo.
Amesema kuwa anashindwa hata afanye nini kuwasaidia hao wazee ikiwa wasaidizi wake ndio wameshindwa kumpa ushirikiano madhubuti wa kuwabaini na kuchukua taarifa za wazee hao.
Hata hivyo amedai kuwa atakachokifanya ni kuendelea kuhimiza suala hili kwa wananchi na viongozi hao ili waweze kuona umuhimu wa kuwasaidia wazee hao ambaoa umri wao umekwenda na hawawezi kufanya chochote zaidi ya kuitaji kusaidiwa zaidi na watu wenye nguvu kama vijana ambao kwa sasa ndio watendaji.
Post a Comment
karibu kwa maoni