0
Rapa Roma Mkatoliki ameachia video ya wimbo wake ‘Zimbabwe’ ukiwa ni wimbo
wake wa kwanza tangu alipotekwa na kuteswa kwa siku tatu.

Kupitia ‘Zimbabwe’ Roma amesimulia tukio la utekaji wake,  watu
anaoamini walimteka na sababu za kuamua kutoendelea kufuatilia jarada la
upelelezi wa tukio hilo.

Mkali huyo pia amezungumzia kitendo cha baadhi ya wasanii wenzake
kutomtembelea alipokuwa anauguza majeraha ya mijeredi ya watesi wake.

Pia, rapa huyo  amezungumzia kauli ya Mbunge aliyedai bungeni kuwa
amemtukana mkuu wa nchi.

Mkali huyo wa mashairi yenye mvuto wa maajabu (Rhymes of Magic
Attraction) amekanusha tetesi kuwa watekaji wake walikuja na Noah huku
akiwachana kuwa waachane na tabia za kutekana na kutumia silaha bali washindane
kwa hoja.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top