0


Tume ya taifa ya uchaguzi Kenya
imemtangaza Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee kuwa mshindi wa
uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne.
Rais Kenyatta alipata kura
8, 203, 290.. ambayo ni asilimia 54 naye mpinzani wake mkuu, mgombea wa
muungano wa upinzani wa National Super Alliance Raila Odinga akapata
kura milioni 6,762,224 ambayo ni asilimia 44.

Akitangaza matokeo
hayo mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC Wafula Chebukati
alisema kuwa ni asilimia 78 ya wapiga kura milioni 19 waliosajiliwa
pekee walioshiriki katika shuguhuli hiyo ya kidemokrasia.

Alisema
kuwa licha ya matatizo machache kukumba mfumo mpya wa kutangazia
matokeo, tume yake ilifanikiwa kutangaza matokeo hayo bila tashwishi
yoyote.

Aliongezea kuwa hatua zilizochukuliwa kuandaa uchaguzi huo ni hakikisho tosha la ukomavu wa kidemokrasia nchini.

Alisema
kuwa Wakenya wengi walijitokeza na kivumilia hali ya anga ili kushiriki
katika zoezi hilo la kidemokrasia kutokana na uaminifu walio nao kwa
tume hiyo ya uchaguzi.

Aliongezea kwamba licha ya kukumbwa na
changamoto chungu nzima katika mahakama waliweza kuandaa uchaguzi huo
kwa njia ya haki uwazi na uhuru,

Akitoa hotuba yake rais Uhuru Kenyatta amewashukuru wafuasi wake na Wakenya wote kwa jumla kwa kumpatia muhula mwengine.

Aidha amemtaka mpinzani wake mkuu Raila Odinga na wafuasi wake
kushirikiana naye katika kujenga Kenya akisema kuwa Uchaguzi huja na
kumalizika lakini wakenya ni sharti wasalie kama mandugu na majirani
wema.

''Katika kila mashindano kuna mshindi na aliyeshindwa
,hivyobasi namuomba ndugu yangu mkubwa Raila Odinga na wafuasi wake
kushirikiana nami katika kulijenga taifa hili kwa sababu uchaguzi huja
na kumalizika lakini wakenya ni sharti wanedlea kuwa majirani wema'',
alisema Uhuru Kenyatta .

Na muda mfupi tu baada ya Uhuru Kenyatta
kutanzwa rais mteule wafuasi wake kote nchini walisherehekea ushindi huo
kwa vifijo na nderemo.

Muungano wa upinzani ulikuwa umepinga utaratibu uliokuwa unatumiwa na tume hiyo kupeperusha matokeo ya uchaguzi huo.

Aidha, viongozi wa muungano huo walikuwa wamedai mitambo ya tume hiyo ilidukuliwa na matokeo kubadilishwa.

Viongozi hao walikuwa Alhamisi wametangaza kwamba mgombea wao, Bw Odinga
ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu katika serikali ya Mwai Kibaki, kuwa
mshindi wa uchaguzi huo.





Matoeko kamili ya wagombea wote kama yalivyotangazwa na Bw Chebukati

Mgombea Chama Kura Asilimia
Uhuru Kenyatta Jubilee 8,203,290 54.27
Raila Odinga ODM 6,762,224 44.74
Mohamed Abduba Dida ARK 38,093 0.25
Japheth Kavinga Kaluyu Mgombea wa kujitegemea 16,482 0.08
Michael Wainaina Mwaura Mgombea wa kujitegemea 13,257 0.09
Joseph Nthiga Nyagah Mgombea wa kujitegemea 42,259 0.28
John Ekuru Aukot Thirdway Alliance 27,311 0.18
Cyrus Jirongo UDP 11,705 0.08
Muda mfupi kabla ya matokeo hayo kutangazwa, Muungano wa upinzani ulikuwa umesema hauungi mkono tangazo la matokeo la IEBC.

Ajenti
mkuu wa muungano huo Musalia Mudavadi alisema malalamiko
yaliyowasilishwa na muungano huo kwa tume hayajashughulikiwa ipasavyo.

Bw
Mudavadi amesema baada ya kukutana na tume hiyo, walifahamishwa kwamba
baadhi ya mambo yao yatashughulikiwa baada ya matokeo kutangazwa.

"Mikutano ilikuwa kama shughuli ya uhusiano mwema tu," amesema.

Tume ilikuwa imewaalika maajenti wakuu kwa mkutano kabla ya kutoa tangazo la matokeo.

Lakini upinzani umesema hautashiriki katika kukubaliana na tangazo la tume hiyo.

Naibu ajenti wa muungano huo James Orengo ametilia shaka waangilizi ambao walikuwa wamesema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.

Amesema waangalizi hao walifaa kuchunguzwa kwanza.

Bw Orengo amesema pia kwamba muungano huo haupangi kwenda kortini kupinga matokeo.

Viongozi
wa kanda ya Afrika Mashariki, wakiwemo Rais wa Rwanda Paul Kagame na
Yoweri Museveni wa Uganda wamempongeza Rais Kenyatta kwa ushindi wake.





Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top