Binti wa miaka 22 aliejifungua mapacha watatu wote wa jinsia
ya kike wilayani Babati mkoani Manyara
na kukimbiwa na mume wake,anaomba msaada kwa wasamaria wema ili aweze
kuwalea watoto hao.
Ambae yupo tayari kumsaidia mama huyo, anaweza kumsaidia
kupitia namba za simu ni 0766 32 02 42.
Leonika Andrea Ni binti mwenye miaka 22 anaeishi katika
kijiji cha Managha kata ya Singe Halmashauri ya mji wa Babati mkoani
Manyara,alihitimu elimu ya Sekondari
kidato cha nne mwaka 2013 katika
shule ya Sekondari Sumaye.
Alibeba mimba ya pili akiwa na mwanaume wake Sigifridi motto wa kike waliompatian jina la Caren,mara
baada ya kubeba ujauzito wa pili mwaka 2016 alikuwa na mahusiano mazuri na huyo
mwanaume wake,siku zikazidi kwenda Leonika Mungu akamsaidia akajifungua mapacha
watatu katika hospitali ya mji wa Babati Mrara ambao walikuwa na kilo moja moja
hivyo kulazimika kuhifadhiwa katika
chumba maalumu cha joto katika hospitali hiyo mpaka walipoongezeka
uzito na hatimaye kuruhusiwa kurejea nyumbani.
Leonika anaishi na mama yake ambaye ni mkulima na
mfugaji,baba ameikimbia familia tangu mwaka 2011 ana aliaga anakwenda mjini
Dodoma kutafuta Maisha lakini mpaka sasa hajaonekana nyumbani na pindi
anaporejea nyumbani ,haji na chochote kama ilivyozoeleka kwamba baba anaporejea
lazima aje na kitu amabacho kitaifurahisha familia.
Mama wa mapacha watatu Leonika Andrea anasema walikutana na
mwanaume huyo Rombo Kilimanjaro na wakakubaliana na kuishi pamoja na kupata
mtoto wa kwanza ,lakini baada ya kujifungua mapacha watatu mwanaume alibadilika
na kurudi kumuiba mtoto wao wa kwanza ambaye ni Carren na mpaka sasa hajui
alipo na namba ya simu kabadilisha.
Mama Leokania anasema kuwa anashindwa hata kufanya vibarua
kwa ajili ya kupata mkate wa kila siku kutokana na kuzidiwa na majukumu haswa
ya kuywalea wajukuu hao kwani binti mwenyewe kwake inakuwa ni vigumu kwa watoto
watatu.
Mama anaomba mwenye kuguswa na jambo hilo wajitolee kwa moyo
chochote walichonacho ili wapte nguvu na kuendelea na shuguli nyingine.
Kwa upande wa majirani nao wamesema wametoa misaada yao
kadri walivyoweza ila bado msaada unahitajika kwa ajili ya kuisaidia familia
hiyo.
Msaada wako ni wa muhimu sana ili uweze kuwasidia watoto hao
kuku vizuri,Kwa yeyote ambaye ataguswa kama binadamu anaweza kumsaidia Leonika
kupitia Mpesa namba za simu ni 0766 32 02
42
Wanasema leo kwake,kesho kwako. Mungu akubariki.
Post a Comment
karibu kwa maoni