0


Serikali imetoa shilingi bilioni 5.6 kwa ajili ya kutengeneza bara bara  yenye urefu wa km 4.108 mjini Babati kwa kiwango cha lami katika kipindi cha mwezi novemba mwaka huu hadi novemba mwakani.

Ujenzi huo utafanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya pili itakuwa ni zaidi ya nusu.

Fedha hizo kutoka serikali zimetolewa kwa mkopo wenye masharti nafuu kutoka bank ya dunia ambapo imetolewa kwa ajili ya kukarabati miji kumi na nane [18] inayoendelea ikiwemo Babati.


Serikali ya Tanzania imeshiriki asilimia mia moja 100% katika kutekeleza hilo katika miji na majiji.


Akizungumza na kituo hiki kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Babati Bashiri  Mhuja amesema tayari wameshafanya makubalianao na mkandarasi atakaejenga bara bara hizo.

Bara bara zitakazopitiwa na lami ni pamoja na Maso mapya Nyerere,Mrombo,Mandela na Hango.

Bara bara hizo zitajengwa kisasa kwa kutengenezwa maeneo ya kuegesha magari [packing] hivyo kuongeza mapato ya halmashauri ya mji wa Babati na mkoa wa Manyara kwa ujumla.

Makubaliano hayo ya ujenzi wa Bara bara ya lami katika mitaa ya mji wa Babati pia yameshuhudiwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Mohammed Kibiki.

Kaimu Mkurugenzi mwanasheria mkuu wa halmashauri,amesema kuwa zipo fursa nyingi zitakazojitokeza pindi ujenzi unapoendelea na kuwataka vijana na wakina mama,mama ntilie kuzitumia vizuri fursa hizo kujikwamua kiuchumi.

Mbali na hayo ametoa angalizo kwa wakazi wa mji wa Babati kujikinga na ugonjwa wa hatari wa ukimwi kwa kuchukua tahadhari.


Wageni wanapokuja huwa wanakuja na mambo mengine na vishawishi vinakuwepo ila naomba wakazi wa mji wa Babati tuchukue tahadhari.Alisisitiza.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top