Hatimaye michuano ya Usalama Cup 2017 Babati Manyara imekamilika leo kwa
City Boys kunyakua kitita cha shilingi milioni moja baada ya kumtoa
Veta Manyara kwa mikwaju ya penati 6-5.
Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara alieandaa michuano hiyo ametoa zawadi kwa washindi na kuwapatia vyeti timu zote zilizoshiriki na kusisitiza jamii kutii sheria bila shuruti,kupiga Vita mimba mashuleni pamoja na kupinga utumiaji wa madawa ya kulevya.
Michuano hii imejenga historia ndani ya Babati kwa kuhudhuriwa kwa wingi na Maelfu ya watu tangu kuanza kwake septemba 16 mwaka huu.
Mshindi wa pili ni Veta Manyara kapata 700,000,wa tatu Kariakoo amepata 500,000 na mshindi Wa nne Stand United amejipatia kitita cha shilingi 200,000.
Baada ya ligi ya usalama cup kimalizika sasa inafuata ligi ya wilaya mapema mwezi novemba ikisimamiwa na kuratibiwa na chama cha soka wilaya ya Babati BDFA.

Post a Comment
karibu kwa maoni