0
Aidha, mvua hizo zilisababisha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kujaa maji zikiwamo nyumba na kusababisha uharibifu wa mali.
MAWASILIANO ya barabara kati ya jiji la Dar es Salaam na mikoani imerejea leo baada ya magari kuanza kupita katika daraja la Kiluvya ambalo jana lilikuwa limejaa maji na hivyo kufungwa kwa ajili ya usalama, anaandika Richard Makore.
Aidha, mvua hizo zilisababisha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kujaa maji zikiwamo nyumba na kusababisha uharibifu wa mali.

Leo mtandao huu wa  umeshuhudia mabasi yaendayo mikoani yakipita katika daraja hilo baada ya vyombo vya ulinzi na usalama kujiridhisha kwamba hakuna madhara yanayoweza kutokea hapo tena.
Jana vyombo hivyo viliyazuia magari yote kupita hapo na hivyo kuelekeza mabasi yaliyokuwa yakitokea mikoa mbalimbali ya bara kupita Bagamoyo ili kuingia jijini Dar es Salaam.

Mvua zilizonyesha juzi na jana mchana zilileta madhara baada ya daraja la Kiluvya linalounganisha mkoa wa Pwani na Dar es Salaam kuja maji na hivyo magari kushindwa kupita.

Kutokana na daraja hilo kujaa maji hudumza za usafiri wa magari ya abiria, mizigo na binafsi ulisitishwa na wananchi wakaombwa kutumia barabara ya Bagamoyo.

Daraja hilo ni kiungo muhimu kati ya jiji la Dar es Salaam pamoja na mikoa mbalimbali ya Kaskazini, Kati, Kanda ya Ziwa, Nyanda za juu Magharibu.

Aidha, mvua hizo zilisababisha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kujaa maji zikiwamo nyumba na kusababisha uharibifu wa mali.

Post a Comment

karibu kwa maoni

Top