Watu wapatao 57 wameuawa baada ya mshambuliaji wa kujitoa
mhanga kujiripua kwenye kituo cha kuwasajili wapiga kura katika mji mkuu wa Afghanistan,
Kabul.
Shambulio hilo limefanyika baada ya siku kadhaa za utulivu
katika mji huo. Watu wengine zaidi ya mia moja walijeruhiwa kwenye shambulio
hilo.
Mauaji hayo yanaweza
kuchelewesha uchaguzi wa bunge uliopangwa kufanyika terehe 20 mwezi Oktoba.
Kundi la magaidi
wanaojiita dola la Kiislamu (IS) wamedai kuhusika na shambulio hilo na hivyo
kuongeza wasi wasi mkubwa juu ya usalama kabla ya kufanyika uchaguzi huo.
Post a Comment
karibu kwa maoni