Hayo yamesemwa na
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), alipokutana na
kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Bi. Katarina Rangnitt,
Jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa,
Serikali imejipanga kulipa madeni kwa wadau mbalimbali baada ya madeni hayo
kuhakikiwa, hata hivyo amesema kuwa hatua za kukopa zitaangaliwa kwa umakini
mkubwa ili kuzuia kuwa na madeni ambayo hayana tija kwa wananchi na Serikali.
Tayari baadhi ya
madeni yameanza kulipwa na Serikali imeendelea kutimiza ahadi zake ilizozitoa
kwa wananchi kwa kuangalia vipaumbele vyenye kuleta matokeo chanya na ya haraka
kwa wananchi, utekelezaji wake unazingatia weledi mkubwa ili kuhakikisha kero
za wananchi zinatatuliwa kwa wakati.
“Aidha katika
kuhakikisha Serikali inaendelea kuwahudumia wananchi ipasavyo, kumekuwa na
mikakati ya kuwaongezea watumishi ujuzi ili kuendana na kasi ya maendeleo
kuelekea uchumi wa kati kwa kuwa tuna uhaba wa watu wenye ujuzi wa kutosha,
hivyo ni vyema wadau wa maendeleo wakalitazama hilo ili kusaidia katika kuharakisha
ukuaji wa uchumi”, alieleza Dkt. Mpango.
Kwa upande wake
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Bi. Katarina Rangnitt amesema kuwa nchi yake
inania ya kusaidia kukuza Sekta ya nishati na tayari mazungumzo na Wizara
husika yameanza.
Alielezea umuhimu
wa Sekta Binafsi katika kukuza uchumi wa nchi ambapo amesema nchini mwake
wafanyabiashara wanachangia pato la ndani kwa asilimia 50 kwa kuwa kuna
biashara huria.
Waziri Mpango
amesema kuwa Serikali inafanyajitihada za dhati kuhakikisha kuna mazingira bora
ya biashara na ili kufikia huko kumekuwa na majadiliano ya mara kwa mara na
wafanyabiashara nchini ambapo kero zao nyingi zimetatuliwa ikiwemo kupungua kwa
uwingi wa kodi.
“Siwezi kuwa Waziri
wa Fedha ikiwa sitakuwa na wafanyabiashara, kwa kuwa wao ndio wanaolipa kodi
zinasosaidia kuendesha nchi”, aliongeza Dkt. Mpango.
Kuhusu utekelezaji
wa Demokrasia na Haki za Binadamu, Dkt Mpango amesema kuwa mambo hayo yapo
kikatiba na Tanzania inafuata katiba na kuiheshimu hivyo haki za binadamu
zinafuatwa kwa mujibu wa sheria na hakuna yeyote anayependa haki zake zivunjwe.
Hata hivyo ameeleza
kuwa ni vema tamaduni za Mtanzania zikaendelea kuheshimiwa wakati wa
utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano wa maendeleo.
Alitoa wito kwa
jamii kuendelea kutangaza yale mazuri yanayojitokeza nchini yakiwemo ya kukua
kwa uchumi kwa kuwa Tanzania itajengwa na watanzania.
“Inashangaza kuona baadhi ya watu wakieleza
mabaya tu ili hali kuna mafanikio mengi yaliyopatikana, tunakaribisha ukosoaji
lakini wenye tija” alifafanua Dkt. Mpango.
Pia, alisema Serikali
inadhamira ya dhati ya kulinda wawekezaji wa ndani lakini amewataka wawekezaji
hao kuungana kwa lengo la kuongeza nguvu na nyenzo bora ili watakapopata fursa
ya kujenga miundombinu na mambo mengine, wafanye kwa ubora unaokubalika na
wenye tija.
Imetolewa na:
Benny Mwaipaja
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
Post a Comment
karibu kwa maoni