0
Ezra ChilobaAfisa mkuu mtendaji wa Tume ya Uchaguzi IEBC Ezra Chiloba amekuwa likizoni. Alikwenda likizo ya wiki tatu baada ya shinikizo kutoka kwa muungano wa upinzani Nasa kumtaka ajiuzulu kuzidi.
Lakini anaonekana kukerwa na tamko la mmoja wa wabunge wa Nasa Junet Mohamed kwamba bado amekuwa wakiingilia uchaguzi wa leo. Amekanusha tuhuma hizo:Anyang' Nyong'oAnyang' Nyong'oAnyang' Nyong'o
Lakini Gavana wa kaunti ya Kisumu, magharibi mwa Kenya, amesema uchaguzi hautarudiwa katika jimbo hilo kama alivyotangaza mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC Wafula Chebukati Jumamosi.
Prof Anyang'a Nyong'o amesema kaunti hiyo itafanya maombolezi ya wiki moja kwa heshima ya watu wawili waliouawa leo.
"Nimetangaza kama gavana wa hii kaunti wiki moja ya maombolezi ambapo wakati huo hakutakuwa na sherehe. Kwetu uchaguzi huwa ni sherehe," amesema.
Amesema iwapo tume hiyo itaendelea kusisitiza uchaguzi ufanyike, basi wataenda kortini kutaka uzuiwe.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top