Wakala wa huduma za bara
bara mkoani Manyara [TANROADS[ wamekabidhi kisima cha maji katika kijiji cha
Boay wilayani Babati mkoani Manyara chenye gharama ya shilingi milioni 42.631.
Mradi huo wa kisima cha maji
katika kijiji cha Boay ni makubaliano kati ya Tanroads mkoa wa Manyara na
kampuni ya ujenzi wa bara bara china
road seventh group L.t.d kutoka nchini China ambayo inajenga bara bara ya lami kutoka
Bonga mkoani Manyara hadi Dodoma.
Akizungumza wakati
anakabidhi kisima hicho kwa mhandisi wa maji halmashauri ya wilaya ya Babati
Samwel Tluway,meneja wa Tanroads mkoani Manyara Bashiru Rwesingisa ameitaka Halmashauri
kukitunza kisima hicho na kukikagua kila mwaka na kuhakiki ubora wa maji.
‘Uchimbaji wa kisima ni moja
kati ya majukumu ya mkandarasi anaejenga bara bara kutoka Mela Bonga-Dodoma,na
kimsingi visima hivyo ni kwa ajili ya kusaidia shughuli za ujenzi wa bara
bara”alisema Rwengisira.
Kisima hiki kilipatikana
baada ya uchunguzi uliofanyika na watafiti wa kijiolojia kutoka chuo cha Maji
Ubungo mwezi oktoba 15, 2015 ambao
waliobaini kuwa maji hayo ni safi na salama kwa matumizi ya bindamu.
Mashine ililiyofungwa
kupandisha maji kutoka ardhini katika Kisima hicho inatumia nishati ya jua
nishati jadidifu ili kuepuka gharama za umeme wa Tanesco.
Mkandarasi huyo amechimba
visima sita katika vijiji vya Manyara na
Dodoma,vijiji hivyo ni
Ukunku,Kolo,Masawi visima viwili,Boay pamoja na Bereko.
Kisima hicho
walichokabidhiwa wanakijiji wa kijiji cha Boay
kina sifa za kipekee, kina uwezo wa kutoa maji hadi lita 6,000 kwa saa,lina
uwezo wa kuhifadhi maji lita elfu hamsini 50,000,pamoja na pampu yenye uwzo wa kupampu
maji lita 2,100 kwa saa.
Mwenyekiti wa kijiji cha
Boay Emmanuel Nikodemus Kaji ameishukuru kampuni hiyo ya China road seventh group Ltd pamoja na serikali kupitia Tanroads kwa kuwapelekea huduma muhimu ya
maji wakazi wa kijiji hicho.
‘Naishuru sana serikali kwa
kutukumbuka wananchi wa vijijini katika huduma muhimu za kijamii kama hizi”.
Akizungumza kwa niaba ya Nao
wakina mama mjumbe wa serkali ya kijiji cha Boay Bi Zamda Fante amesema kisima
hicho kitawasaidia kuwapunguzia usumbufu waliokuwa wanaupata kutafuta maji
umbali mrefu.
Alisema kwa kapatiwa kisima
hicho cha maji watapata nafasi ya kufanya zaidi kilimo cha umwagiliaji.
Pia amewataka wanakijiji
wenzake waulinde mradi huo waliopewa kama zawadi na kampuni hiyo ya ujenzi wa
bara bara kutoka nchini china.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugezi wa Halmashauri ya wilaya ya Babati mhandisi wa maji Samwel Tluway amewahidi wakandandarasi pamoja na Tanroads kuwa mradio huo wataulinda,kuendeleza na kuuboresha zaidi.
Meneja mradi wa kampuni ya
China Road Seventh Group[CRSG] Bwana Dong Hui ameishukuru Tanroad Mkoa wa
Manyara kwa kuwapa ushirikiano katika kipindi chote walichokuwa wakitengeneza
bara bara hiyo kutoka Mela bonga mpaka Dodoma ambapo kwa sasa imekamilika na
inatarajiwa kuzinduliwa na rais wa Tanzania John Magufuli kati ya mwezi oktoba
na Novemba mwaka huu.
Post a Comment
karibu kwa maoni