Waziri wa mambo ya ndani Dr.Mwigulu Lameck Nchemba amewataka
watumishi wa Mungu na watanzania kwa ujumla kumuombea rais John Pombe Magufuli
katika kazi ngumu anayoifanya ya kuitengeneza nchi.
Dr.Nchemba ameyasema hayo jumamosi 25 novemba wakati akizungumza na waumini wa kanisa
la KKKT mtaa wa Babati mjini Mkoani Manyara katika ibada maalumu ya changizo la
ujenzi wa jengo la kisasa l akanisa katika mtaaa huo.
Naye askofu wa kanisa la KKT
jimbo la kaskazini kati Dr. Solomon Jacob Masangwa amemfananisha rais
Magufuli na mhasisi wa kanisa la Lutheran Duniani Martin Luther ambaye
alipingwa na watu waovu katika kufanya ujenzi wa kanisa huku akimtaka
asivunjike moyo.
Askofu Masangwa ameeleza kuwa kazi anayoifanya rais Magufuli
ni kubwa hivyo watanzania wanapaswa kumuombea na kumuunga ili kukamilisha ujenzi wan chi hii.
Wanaompinga rais Magufuli katika kazi hii kubwa anayoifanya
nawafananisha na wale waovu waliokuwa wanampiga vita Martin Luther wakati
alipokuwa analijenga kanisa.
Katika harambee hiyo Dr. Nchemba alitoa shilingi milioni
kumi katika kuunga mkono ujenzi wa kanisa hilo la kisasa.
Naye mbunge wa viti maalum mkoa wa Manyara Ester Alexender Mahawe
akachangia shilingi milioni moja ili kufanikisha ujenzi huo.
Jumla ya fedha zilizopatikana katika harambee hiyo na
zilizokuwepo benki ni shilingi milioni 80,
Jengo hilo kubwa la kisasa litakalogharimu zaidi ya shilingi
milioni mia tano themanini [580] za kitanzania lenye gorofa moja lina uwezo
wa kuingiza watu 3,000.
Post a Comment
karibu kwa maoni