Wanasayansi wanasema kwamba ziwa
kubwa zaidi lenye maji tulivu barani Afrika Victoria linalounganisha
nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, lipo katika hatari kubwa ya kukauka.
Wanasema kwamba uvuvi haramu na uliopitiliza pamoja na uvamizi wa mazingira kuzunguka maeneo ya ziwa ni sababu kubwa.Maji machafu pia yanayotiririshwa kuelekea kwenye ziwa yanahatarisha usalama wa viumbe vya majini.
Mwandishi wa BBC anasema jeshi la Uganda limeweka mipango maalum ikiwa ni pamoja na kuharibu nyenzo za uvuvi zinazotajwa kuwa miongoni mwa sababu.
Post a Comment
karibu kwa maoni