0
Wavuvi wavuta maboti yao ufukweni mwa bahari wakati moshi mkubwa umetanda angani kutokana na volkanoTakriban watu laki moja karibu na mlima Agung kisiwani Bali wametakiwa kuhama wakati maafisa wanahofia mlima huo wa volkano kulipuka pakubwa.
Maafisa Indonesia wameongeza kiwango cha hatari na kupanua zaidi eneo linalokaribiana na mlima huo wa vokano unoendelea kuchemka linalotarajiwa kuathirika.
Uwanja wa ndege wa kipekee katika kisiwa hicho maarufu cha utalii cha Bali umefungwa.
Majivu na moshi wa Volcano hiyo imefikia urefu wa zaidi ya mita 3400 juu ya mlima huo hali iliyosababisha giza.
Mlima huo uitwao Agung ulirusha majivu mengi na kutandaza mvuke na moshi mwingi mara ya pili katika kipindi cha wiki moja.
Maafisa wamehimiza na kuwasaidia maelfu ya wakaazi na watalii kulihama eneo hilo na kwenda kwingine.
Mlima huo wa volkano ulionekana ukitoa moshi na sauti za milipuko zilisikika kwa umbali wa kilomita 12 kutoka juu ya mlima huo.
"Miale ya moto inazidi kutizamwa usiku kucha. Hii inaashiria uwezekano wa mlipuko mkubwa zaidi ," imesema taarifa ya bodi ya kitafa ya usimamizi wa majanga Indonesia, katika ukurasa wake wa Facebook.
Mwaka 1963 mlima huo ulilipuka na kusababisha vifo vya takriban watu 1,600.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top