0
Mwenyekiti wa CCM, Rais John MagufuliMWENYEKITI wa CCM, Rais John Magufuli ameunda Tume ya watu tisa kufuatilia mali za Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchi nzima.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, iliyotolewa Dar es Salaam jana, tume hiyo itaongozwa na Dk Bashiru Ali Kakurwa ambaye atakuwa Mwenyekiti huku Wajumbe wakiwa Walter Msigwa, Albert Msando, Galala Wabanhu ‘Hananasif’, Albert Chalamila, William Sarakikya, Komanya Kitwara, Dk Fenella Mukangara na Mariam Mungula.
“Tume hii itafuatilia mali za chama popote zilipo na itamhoji kila mtu anayehusika katika chama na serikali,” alisema Polepole. Alisema Tume hiyo itakwenda kuhoji watu wote na viongozi na watendaji wa CCM katika mikoa, wilaya, kata, matawi na mashina na aliwataka viongozi katika ngazi hizo, kutoa ushirikiano kwa wajumbe wa tume hiyo. “Natoa mwito kwa Watanzania wanaoshikilia mali za CCM, wajitokeze na waseme ukweli kwa maslahi ya CCM,” alisisitiza Polepole.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top