0


Image may contain: 3 people, people smiling, people standing, child and outdoorWananchi Gendabih Na Dawar Wilaya Ya Hanang katika mkoa wa Manyara Wamempa Heko mkuu wa wilaya Bi. Sara Msafiri kwa Utatuzi wa  Kero Ya Maji  hukuWakisema kuwa imepita Miaka mingi,Wamepita wakuu wa wilaya wengi ambao wamejitahidi kadri wawezavyo kutatua changamoto ya maji ikashindikana.
Lakini Kilio hicho kimekuja kupata dawa mwaka 2017 baada ya kuingia Sarah Msafiri alipochaguliwa na Mheshimiwa Dr. John Pombe Magufuli.

Wakazi wa vijiji  wanaeleza kuwa ugumu huo ulikuwa ukisababishwa na baadhi ya viongozi wa vijiji na vitongoji kwa Kuwachonganisha Wanakijiji na hata kupelekea vijijiji kwa Vijiji kushikiana Mapanga Kugombea Maji Miaka Iliyopita.

Katika kuhakikisaha kuwa wananchi wa Hanang wanapata huduma nzuri za maji Mkuu Wa Wilaya aliamua kutangaza Kuvunjwa kwa  Mamlaka Ya Maji Inayoundwa Na Vijiji Hivyo kuwa Iundwe Upya kwa Udhaifu Mkubwa na uzembe unaoonekana  Ndani Ya Mamlaka Hiyo.
Ikumbukwe kuwa Bi.Sarah Msafiri ndiye mkuu wa wilaya pekee ndani ya mkoa wa Manyara ambaye anaendelea kutatua changamoto mbalimbali za wakazi wa wilaya yake kwa kuitisha mikutano na kushughulikia migogoro iliyopo katika kupatiwa ufumbuzi.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top