Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU inamshikilia Rais mstaafu wa
Chama Cha walimu Tanzania (CWT) Gracian Mkoba kwa tuhuma za rushwa.
Hilo
limethibitishwa na Afisa Uhusiano wa TAKUKURU Makao Makuu, Mussa
Misalaba, ambaye amesema wanamshikilia Mkoba kwa tuhuma za kugawa fedha
kwa baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho ili kuwashawishi
wamchague mgombea anayemtaka.
"Mukoba
ameshastaafu, lakini kuna mgombea mmoja alikuwa anataka achaguliwe,
tumemkamata leo asubuhi akigawa rushwa kuwashawishi wapiga kura kwenye
ukumbi wa Chimwaga wamchague huyo mgombea wake," amesema Misalaba.
Misalaba ameongeza kuwa TAKUKURU inaendelea kufanya uchunguzi zaidi dhidi ya Mukoba kabla ya kumfikisha mahakamani.
Mukoba
anakuwa mtu wa tatu kukamatwa na TAKUKURU kwa tuhuma za rushwa kwenye
uchaguzi ndani ya wiki moja, wengine ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa
Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Sadifa Juma Khamis na
mfanyabiashara Haider Gulamali.
Post a Comment
karibu kwa maoni