Ahadi ya
Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya
kikwete aliyoitoa wilayani Mbulu mkoani
Manyara, wakati wa kampeni ya kugombea urais mwaka 2005 ya kujenga daraja la
mto Magara ili kuunganisha wilaya hiyo
na makao makuu ya mkoa wa Manyara
Babati, imeanza kutekelezwa.
Ni baada ya
kukamilika kwa Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa
daraja hilo lenye upana wa mita 84 pembeni 24 na katikati mita 36 lililoko
umbali wa kilomita 21 kutoka barabara
kuu ya Babati – Arusha, tayari jana Mkandarasi aliyeshinda zabuni ametia saini
ya ujenzi wa kivuko hicho.
Akisoma
taarifa ya mradi huo mbele ya mwanasheria wa serikali Bi. Emakulata Banzi,
wahandisi wa wakala wa barabara TANROADS na wawakilishi wa mkandarasi
aliyeshinda zabuni,Meneja wa TANROADS Mhandisi Bashiri alisema Serikali
Ilitenga fedha kuanzia mwaka 2007/2008, huku ikiendelea na matengenezo ya
maeneo korofi ya mlima Magara.
Alisema
Barabara hiyo kupitia daraja hilo ni muhimu kiuchumi kwani imeunganisha hifadhi
za taifa za Manyara na Tarangire kwa kupitia Mayoka na kuunganisha mashamba
makubwa ya mpunga, mahindi na miwa yaliyopo upande wa pili wa mto kuelekea soko
lililoko Babati na Arusha.
Daraja hilo
litamalizi kero ya wanafunzi kukosa masomo wakati wa masika, kwani mto huo
hujaa maji na husababisha wanaoishi ng’ambo kushindwa kuvuka upande wa pili
Taarifa hiyo
iliendelea kwa kusema kuwa zabuni ya ujenzi zilitangazwa tarehe 28 Machi 2017
kwa makandarasi wazalendo na kufunguliwa tarehe 28 Aprili 2017, baada ya
uchambuzi wa zabuni aliependekezwa alikuwa M/s Roctronic Limited wa Moshi na
hatimaye kujitoa tarehe 02/Juni 2017
kutekeleza mradi huo kwa madai ya kukosa baadhi ya vitendeakazi.
Hatimaye
zabuni ilitangazwa kwa mara ya pili ikishirikisha makandarasi wa kimataifa
ambapo Mkandarasi M/s China Railway Seventh Group Co. Ltd alipendekezwa kupewa
kazi hiyo kwa gharama ya Tsh. Milioni 12,641.244 na mkataba kusainiwa tarehe 14
Desemba 2017 kazi itakayofanywa kwa miezi 24.
Post a Comment
karibu kwa maoni