Wasaidizi wa
sheria wametakiwa kuendelea kuwasadia wananchi katika kujua sheria ili
jamii iishi kwa kutambua haki zao za
msingi.
Akizungumza
na wanasheria na wasaidizi wa sheria mkoa wa Manyara waliokutana leo mjini
Babati katika tamasha lao linalofanyika kila mwaka,mkuu wa wilaya ya Babati
Raymond Mushi amesema kila mwananchi akiitambua sheria itasaidia kupungua kwa
vitendo vya uhalifu katika jamii.
Hata hivyo
mkuu wa wilaya Mushi amezindua
tovuti rasmi ya shirika la
MACSNET pamoja na jarida la msaada wa kisheria
itakayosaidia kumpatia mwananchi taarifa mbalimbali na kazi zinazofanywa
na shirika hilo.
Hata hivyo
mkuu wa wilaya Mushi amezindua
tovuti rasmi ya shirika la
MACSNET pamoja na jarida la msaada wa kisheria
itakayosaidia kumpatia mwananchi taarifa mbalimbali na kazi zinazofanywa
na shirika hilo.
Mwanasheria wa
Asasi ya MACSNET Eliakim Paulo amesema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja
wamejitahidi kuwajengea uwezo wasaidizi wa sheria ili nao wakatoe msaada kwa
wananchi katika kujua sheria.
Aidha
ameeleza kuwa lengo la kuanzisha mradi huo mwanzoni mwa mwaka huu ni kuwapatia
elimu wasaidizi wa sheria ili kupunguza migogoro ya ardhi zaidi ya asilimia 90
iliyopo maeneo mbalimbali ya mkoa wa Manyara.
Eliakimu
amesema kuwa kupitia elimu wanayoitoa kwa wasidi hao wa sheria itasaidi katika
kupunguza migogoro mbalimbali ambayo inayotokana na kutokujua sheria.
Anna Emanuel
Fisoo afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Manyara anasema kuwa kwa tamasha hilo
linafungua njia mpya ya kuwasaidia wakina mama na watoto ambao kwa kiwango
kikubwa ndio walengwa wa matukio ya vitendo vya ukatili.
Amesema Wanawake
wengi mkoa wa Manyara wamekuwa wakiteseka
kwa kudhulumiwa haki zao haswa ardhi kwa kutokujua sheria.
Amesema
idara ya ustawi wa jamii kwa kushirikiana na dawati la jinsia polisi,vyombo vya
habari na wasaidizi wa sheria wanafanya kazi kubwa ili kutokomeza vitendo vya kikatili
katika jamii.
Msaidizi wa
sheria kutoka wilaya ya Hana’ng kijiji cha Balangdalalu Raheli Araja amesema
kesi nyingi wanazokutanazo wakiwa katika utekelezaji wa majukumu yao ni kesi za
ubakaji na ukeketaji lakini jamii kutokana na kukosa elimu ya sheria hazifiki
katika vyombo vya sheria hali inayopelekea matukio kama hayo kuendelea kuwepo.
Bi Anna
Fissoo akizungumzia suala la hilo la ubakaji na ukeketaji katika mkoa wa Manyara amesema kuwa baadhi ya
watu wamekuwa wakiogopa kutoa ushahidi mahakamani na wengine kumalizana kimila
hali inayopelekea mahakama kushindwa kuwatia hatiani wahusika.
Aidha wasaidizi
hao wa sheria wamishukuru serikali kwa kutambua mchango wao katika jamii na
kuahidi kushirikiana nao huku wakitoa wito kwa wananchi kuwa wapendane na
kuacha kugombea ardhi ambayo kwa sasa imekuwa ikisababisha migogoro baina ya
mtu na mtu na wilaya kwa wilaya hata mkoa kwa mkoa.
Gidamis
Shahanga amesema kwa sasa ardhi inazidi kuwa ndogo na matumizi ya ardhi
yanaongezeka na idadi ya watu pia inaongezeka hivyo wanachi wafuate taratibu za
umiliki ardhi.
Tamasha hilo
limejumuisha wawakilishi kutoka katika
wilaya 5 za mkoa wa Manyara ambao walipata nafasi ya kuwasilisha taarifa za kazi za mwaka kwa kila wilaya kwa kupitia wawakilishi hao
na kupata muda wa kuuliza maswali na kujadili kutokana na taarifa hizo. Wilaya
hizo ni Hanang, , Babati, Kiteto, Mbulu na
Simanjiro.
Post a Comment
karibu kwa maoni