0
mediaKiongozi wa kundi la kigaidi la Boko Haram nchini Nigeria, Abubakar Shekau kwa mara nyingine, ameonekana katika mkanda wa video akisifia wapiganaji wake kutekeleza mashambulizi ya kigaidi kipindi cha shamrashamra cha Krismasi na mwaka mpya.
Huu ni mkanda wake wa kwanza kuonekana baada ya miezi kadhaa, hata baada ya jeshi la Nigeria kudai kuwa walikuwa wamemuua.
Katika mkanda huo wa dakika 31, Shekau amesema ana afya nzuri na hakuna kilichompata kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa.
Akizungumza kwa lugha ya Kihausa, Shekau amesisitiza kuwa jeshi la Nigeria na Polisi, hawawezi kumfanya lolote licha ya taarifa wanazotoa mara kwa mara.
Kiongozi huyo wa Boko Haram amesifia wapiganaji wake kwa kutekeleza mashambulizi ya kigaidi katika miji ya Maiduguri, Gamboru, na Damboa kipindi chote cha shamrashmara ya Krismasi na mwaka mpya.
Mamia ya watu walipoteza maisha Kaskazini mwa Nigeria, katika miezi miwili ya mwisho wa mwaka 2017.
Serikali ya Nigeria ikisaidiwa na mataifa jirani, bado haijafanikiwa kulimaliza kundi hilo lililoanza mashambulizi yake mwaka 2009.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top