Afisa
Mchambuzi Mifumo ya Kompyuta Ndg. Psalm Kisuda akitoa Kitambulisho cha Taifa
kwa Bi Rabia aliyekamilisha Usajili awali na kukamilisha hatua zote ikiwemo ya
Uhakiki na Uwekaji Pingamizi.
|
Hatua
hiyo inamhusisha mwananchi kuhakiki
taarifa zake juu ya maombi ya Kitambulisho cha Taifa aliyoyafanya awali zilizobandikwa kwenye vituo vya Usajili katika
kata, mitaa na vijiji wanakoishi.
Taarifa
ambazo mwananchi atatakiwa kufika na kuzihakiki ni zinazohusu: Makazi,
Uraia, Umri, Jinsi, Picha na Jina la Mwombaji iwapo zinasomeka kwa usahihi.
Bi. Catherine
Makuri Afisa Usajili, wilaya ya Singida ambaye pia ni mratibu wa shughuli za
Usajili Mkoani Singida amesema katika mkoa wake kwa sasa wameingia katika hatua
ya tatu ya Usajili inayojulikana kama Uwekaji Pingamizi ambapo mwananchi
anapata fursa ya kuhakiki taarifa zake alizozijaza za Uraia, Umri, Picha, Jinsi
na Makazi ya mwombaji sambamba na kuhakiki taarifa za waombaji wengine kama
ziko sahihi na kuwafichua wadanganyifu wote endapo atabaini kuwepo kwa waombaji
waliodanganya taarifa za uraia wao kwa kujifanya ni raia na kumbe sivyo.
Aidha Bi
Makuri Amewataka wananchi wote wa mkoa wa Singida ikiwemo wa Halmashauri ya
Manispaa ya Singida katika kata za Mughanga, Mitunduruni, Minga, Utemini, na
Ipembe ambazo zoezi hili limeanza kujitokeza kwa wingi kuhakikisha wanahakiki
taarifa zao ili Vitambulisho vitakapotolewa viwe vimebeba taarifa sahihi ya
waombaji.
Zoezi la
Uwekaji Pingamizi katika wilaya ya Ikungi kata za Iyumbu, Ighombwe, Mwaru,
Irisya, Mang`onyi, Unyahati, Dungunyi na Ikungi linaendelea vizuri na wananchi
wamejitokeza kuhakiki taarifa zao.
Watendaji wa Vijiji tunaendelea kushirikiana
nao kutoa taarifa kwa wananchi ili wafike kwenye vituo vya Usajili ambapo
taarifa hizo za waombaji kwa ajili ya Kuweka Pingamizi zimebandikwa. Ameyasema
hayo Afisa Msajili Wilaya ya Ikungi Bi Agnes Mtei.
Bi Neema
Chaurembo Afisa Msajili wilaya ya Mkalama ameeleza kuwa kwa wilaya yake
wamekamilisha Usajili katika Kata sita za Mwanga, Mkalakala, Ilunda, Kikhonda,
Kinampundo na Nduguti ambapo maandalizi ya kuwezesha kuanza kwa zoezi la
Uwekaji pingamizi katia wilaya yake yako katika hatua ya mwisho hivyo mwanzoni
mwa wiki ijayo taarifa za uwekaji pingamizi zitakuwa zimeshabandikwa kwenye
kata zote.
Kwa wilaya
ya Manyoni zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa mfumo wa mkupuo
limeshakamilika. Katika kata ambazo bado kufikiwa za mkoa wa Singida zikiwemo
na zile za wilaya ya Iramba zitafikiwa karibuni hivyo waandae viambatanisho
muhimu na vya kutosha vinavyohitajika katika Usajili Vitambulisho vya Taifa.
Zoezi
la Usajili wa Mkupuo linafanyika mkoani Singida kwa kwa awamu kwa kata ili kutoa fursa kwa
wananchi kuweza kuendelea na shughuli za uzalishaji hususan kilimo kwa walio
vijijini.
Post a Comment
karibu kwa maoni