Kuanzia asubuhi na mapema leo, Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire
alitupia mtandaoni picha ikimuonyesha akiwa amevaa kandambili za kijani
na njano, halafu hakueleza kitu.
Baada ya kuona picha yake hiyo imesambaa sana, Bwire aliamua kutoa ufafanuzi kwa nini amevaa kandambili za njano na kijani.
"Hizi nilizokanyaga ni za kukanyagia, leo tunakanyaga".
Kumbuka leo, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga wanawavaa Ruvu Shooting wakiwa wenyeji wao jijini Dar es Salaam.
Baada ya kutafutwa na SALEHJEMBE, Bwire amesisitiza kuwa kweli "wanakanyaga".
"Kweli wakati mwingine nimekuwa nikisema lakini haitokei, lakini leo hatutakuwa na utani.
"Tuna kikosi bora na walimu wetu wameangalia makosa ya Yanga. Hivyo tutakachofanya ni kumaliza kazi kupitia kikosi chetu bora."
Yanga iko katika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na
pointi 22 huku Shooting wakielea katika nafasi 15 wakiwa na pointi 11,
tofauti ya pointi 11 dhidi ya Yanga.
Post a Comment
karibu kwa maoni