Mwandishi
mkongwe na mpigapicha maarufu zikiwemo zile za michezo, Athumani Hamisi
Msengi atazikwa kesho mchana kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es
Salaam.
Athumani
amefariki dunia leo katika Hospitali ya Muhimbili baada ya kuugua kwa
muda wa takribani miaka 10 baada ya kupata ajali ya gari akiwa Kibiti
mkoani Lindi.
Taarifa
iliyotolewa na familia inaeleza, Hamisi atazikwa kwenye makaburi ya
Kisutu baada ya mchusho wa Ijumaa na maandalizi yamekuwa yakiendelea.
Athumani alipata ajali hiyo Agosti 12, 2008 katika eneo hilo wakiwa na waandishi wenzake njiani kwenda Kilwa.
Baada
ya hapo alibaki kitandani kwa matibabu Muhimbili, baadaye nchini Afrika
Kusini hadi aliporejea nyumbani akiwa na anatumia kiti kutembelea.
Taarifa
kutoka kwa ndugu zake zinasema jana mchana alizidiwa ghafla,
wakampeleka Muhimbili ambalo alipata matibabu hadi mauti yanamkuta.
Post a Comment
karibu kwa maoni