Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe ametoa wito
kwa watanzania kujitokeza kumchangia msanii wa Filamu Wastara Issa ili
aweze kwenda kupatiwa matibabu India ya mguu wake unaomsumbua.
Mheshimiwa
Mwakyembe ametoa wito huo alipokwenda kumtembelea msanii huyo wa filamu
nyumbani kwake jana Tabata Sanene jijini Dar es Salaam kutokana na
msanii huyo kuwa anasumbuliwa na mguu wake uliyokatwa mpaka kufikia
kuhitajika kufanyiwa upasuaji mwingine.
“Ndugu
zangu watanzania najua kutoa ni moyo na siyo utajiri ninawaomba
mjitokeze kwa kumsaidia msanii huyo kwani mpaka sasa anahitaji kiasi cha
milioni kumi na nane kwa ajili ya kufanikisha safari yake hiyo ya
kwenda kupata matibabu na anatarajia kwenda kwenye matibabu hayo mwezi
ujao,”Dkt.Mwakyembe.
Naye
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi.Joyce Fissoo alitoa wito
kwa wasanii wote wa filamu nchi kujitokeza na kumsadia mwanatansia
mwenzao wa filamu katika kufanikisha anapata matibabu ili aweze kurudi
na kuendelea kufanya kazi zake kama kawaida .
“Bodi
ya Filamu nchini kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa laTaifa tumetoa
kiasi cha shilingi Milioni moja kwa ajili ya kumchangia katika
kufanikisha safari yake ya matibabu na serikali kwa ujumla inafanya
jitihada mbalimbali katika kuhakikisha msanii huyu anapata kiasi hicho
cha pesa kilichobakia,”Bibi Fissoo.
Pamoja
na hayo Katibu Mtendaji BASATA Bw.Godfrey Mngereza alitoa wito kwa
wasanii wote nchini kwa nao kijitokeza kumchangia msanii huyo kwani
wasanii wote ni wamoja kwa maana wote ni wanafanya kazi ya sanaa hivyo
ni vyema kuwa na mshikamano na kusaidiana.
Kwa
upande wa msanii Wastara Issa aliishukuru serikali kwa kumtembelea na
kumjulia hali pamoja na kumchangia na kusema imekuwa nifaraja kubwa
kwake kuwaona na alitoa akaunti namba anayotumia kwa ajili ya
kukusanyanyia michango ambayo ni EQUITY BENKI – 3007111415583 na namba
za simu anazotumia kuchangisha ni 0768 – 666 113 na 0713 666 113 na
alieleza amesajiliwa kwa jina la Wastara Issa katika namba hizo za simu
pamoja na akaunti namba yake.
Post a Comment
karibu kwa maoni