Hoteli Intercontinental, Kabul mnamo Januari 21, 2018 baada ya shambulizi la Taliban lililoua watu zaidi ya 40.REUTERS/Omar Sobhani
Watu
zaidi ya 40 waliuawa katika shambulio la hoteli ya Intercontinental
mjini Kabul mwisho wa wiki iliyopita, ikiwa ni pamoja na raia 25 kutoka
Afghanistan na wageni 15, kulingana na vyanzo vya Afghanistan na
kidiplomasia.
"Ripoti ya mwisho
inasema watu 25 kutoka Afghanistan waliuawa katika shambulio la hoteli
Intercontinental," msemaji wa wizara ya Afya, Wahid Majrooh, ameliambia
shirika la habari la AFP leo Alhamisi, akiongeza kuwa raia wa kigeni 15
wamethibitishwa na balozi zao na serikali zao. Raia wanne kutoka
Marekani ni miongoni mwao, wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilitangaza
jana Jumatano jioni.
"Hatujishughulishi na majeruhi wa kigeni," amesema Majrooh, akiongeza kuwa waliojeruhiwa raia 12 wa Afghanistan pia walipokelewa katika hospitali za serikali zinazosimamiwa na wizara hiyo.
Wageni, waliokufa au kujeruhiwa, walipelekwa kwenye hospitali ya kijeshi ya Kabul au ile ya NDS, idara ya ujasusi ya Afghanistan.
Kwa jumla, raia kutoka mataifa kumi na sita tofauti walikuwepo jioni ya siku ya shambulio la hoteli Intercontinental (inayomilikiwa na serikali ya Afghanistan), ambayo tayari ilishambuliwa mwaka 2011 , kulingana na chanzo cha usalama.

Post a Comment
karibu kwa maoni