Mtu mmoja ambaye hajafahamika anaekadiriwa kuwa na umri wa
miaka 30-40 amekutwa akiwa amekufa katika kijiji cha Haraa kata ya Bonga
wilayani Babati Mkoani Manyara.
Mwili huo umegundulika jana katika kijiji hicho.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kijiji cha Haraa John Bura
Masawe ambaye ametoa taarifa hiyo amesema mwili huo waliukuta ukiwa tayari
umeaharibika vibaya huku Madaktari wakishauri uzikwe katika eneo hilo kwa kuwa mwili ulishaanza
kuharibika na haufai kubebwa.
Hata hivyo mwili huo umezikwa leo Februari 27.2.2018 katika kijiji hicho huku kukiwa hakuna taarifa zozote kutoka kwa ndugu au jamaa wa marehemu huyo.
Kamanda wa polisi
mkoa wa Manyara Agustino Senga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza
kuwa 'inawezekana mtu huyo ameuawa sehemu nyingine na kuja kutupwa katika kijiji
hicho.
Senga amewataka wananchi kushirikiana na jeshi la polisi
kuweza kufichua wahalifu ili mkoa wa Manyara uzidi kuwa salama'.
Post a Comment
karibu kwa maoni