Mkuu wa wilaya ya Babati Mheshimiwa Raymond Mushi akikabidhi mkataba huo kwa mkurugenzi wa BAWASA Mhandishi Iddy Yazidi Msuya. |
Wanakijiji wa Nakwa kata ya Bagara mjini Babati kuanza
kufurahia huduma za maji baada ya Halmashauri ya mji kuukabidhi mradi wa maji
wenye thamani mya shilingi Milioni 806,575,730 kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Babati [BAWASA]
hii na kushuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya
Babati Raymond Mushi na Mkurugenzi wa mji Fortunatus Fwema.
Mkurugenzi wa Bawasa Eng. Iddy Yazidi Msuya amesema kuwa
Mradi huo umekabidhiwa katika mikono salama hivyo wakazi wa Nakwa wanaopata shida ya Maji kwa
muda mrefu wategemee huduma safi za maji saa 24.
Amewaeleza wakazi hao kuwa wataanza kufurahia huduma za
BAWASA ndani ya wiki mbili baada ya kukagua na kuyatazama yale maeneo korofi
katika upatikanaji wa maji.
Eng. Msuya amesema jukumu lao ni kuhakikisha wakazi wa Nakwa
wanapata maji hivyo wananchi watoe ushirikiano katika kutunza miundo mbinu
iliyopo na kutoa taarifa pindi wanapoona bomba linavuja.
Mkuu wa wilaya ya Babati Eng.Raymond Mushi akizungumza na wakazi wa Nakwa. |
Mradi huu wa maji
uliotekelezwa na Halmashauri ya Mji wa Babati na serikali kuu pamoja na
bank ya dunia [WB] ulianza kutekelezwa Novemba22 Mwaka 2013 na kukamilika July 26 Mwaka 2017.
Aidha mradi huo unawahudumia wakazi wa Nakwa wapatao 6,688
chenye vitongoji vitano vyaa Sumbi Kayto,Magara,Mageni na Simbay.
Mpaka kukamilika kwa mradi huu imetumika shilingi Milioni
806,575,730 kutoka serikali kuu na shilingi
Mlioni 5 nguvu za wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Babati Raymond Mushi ameeleza kuwa
aliukagua mradi huo vizuri kwa kushirikana na mkurugenzi wa BAWASA Eng. Iddy
Yazidi pamoja na mkurugenzi wa mji wa Babati Fortunatus Fwema na kumuagiza
mkandarasi kurekebisha kasoro zilizopo katika mradi huo.
Mkuu wa wilaya
akiongozana na wataalamu wa maji alitembea kwa miguu Kilometa 37 kukagua
kasoro zilizopo katika mradi huo huku akiwapongeza wananchi waliogundua kasoro
kwenye mradi huo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Babati Raymond Mushi
amesema kuwa mradi huo kwa awamu ya kwanza
ulikumbwa na harufu ya ufisadi na kwa sasa Taasisi ya Kuzuia na
kupambana na Rushwa [TAKUKURU] inaendelea na uchunguzi hivyo wananchi watoe
ushirikiano pindi wanapohitajika kutoa ushahidi na taasisi hiyo.
Post a Comment
karibu kwa maoni