
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli leo tarehe 14 Februari, 2018 amemteua Meja Jenerali
Yakubu Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ).
Pamoja na uteuzi huo, Mhe. Rais Magufuli amempandisha cheo kutoka Meja Jenerali na kuwa Luteni Jenerali.
Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed anachukua nafasi ya Luteni Jenerali James Alois Mwakibolwa ambaye amestaafu.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewapandisha vyeo kutoka Brigedia Jenerali na kuwa Meja Jenerali wafuatao;
- Brig Jen. J.G. Kingu
- Brig Jen. M.S. Busungu
- Brig Jen. R.R. Mrangira
- Brig Jen. B.K. Masanja
- Brig Jen. G.T. Msongole
- Brig Jen. A.F. Kapinga
- Brig Jen. K.P. Njelekela
- Brig Jen. A.S. Bahati
- Brig Jen. M.E. Mkingule
- Brig Jen. S.S. Makona
Mabrigedia Jenerali wote waliopandishwa vyeo watapangiwa vituo vya kazi baadaye.
Mnadhimu
Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed ataapishwa kesho
tarehe 15 Februari, 2018 saa 5:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
14 Februari, 2018
Post a Comment
karibu kwa maoni