
Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kiongozi wa chama hicho katika Kata
ya Hananasif, Daniel John amefariki dunia katika mazingira ya
kutatanisha.
Mbowe akizungumza na waandishi wa habari jana Februari 13,2018 alisema John alitoweka siku moja iliyopita.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hana
taarifa hizo lakini anawasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kinondoni.
Amesema baada ya mawasiliano atatoa ufafanuzi leo Februari 14,2018.
Mbowe alisema John ambaye ni katibu kata alitoweka akiwa na Reginald Mallya ambaye alijikuta yupo ufukweni mwa bahari.
Mbowe
alisema walitoa taarifa polisi kuhusu kutoweka kwa John na kwamba,
walipokwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) walielezwa kuna mwili
ulipelekwa na polisi.
Alisema
mwili huo ulitambuliwa na mkewe John na una michubuko inayoashiria
alikabwa, una jeraha la panga kichwani na upande mmoja wa kichwa
umebonyea kuashiria alipigwa na kitu kizito.
Kuhusu Mallya alisema alipigwa panga kichwani na alivunjwa mkono. Mbowe ametaka polisi kufanya uchunguzi wa tukio hilo.
Mallya
aliyekuwapo kwenye mkutano huo na waandishi wa habari alisema walikuwa
wakitembea na John ndipo waliposimamishwa na kuingizwa ndani ya gari.
Alisema
alipigwa hadi kupoteza fahamu na alipozinduka alijikuta ufukweni
alikojikokota hadi barabarani ambako alipata msaada wa bajaji na
alikwenda Hospitali ya Mwananyamala alikotakiwa kuwa na taarifa ya
polisi ambayo aliipata Kituo cha Polisi Oysterbay.
Post a Comment
karibu kwa maoni