Mzee Kingunge alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam takriban mwezi mmoja uliopita.
Mke wa Kingunge Peras Ngombalemwiru alifariki dunia mwanzoni mwa mwezi January kutokana na ugonjwa wa kupooza kipindi ambacho Mzee Kingunge alikuwa tayari anapatiwa matibabu ya majeraha hayo.
Mzee
Kingunge alikuwa kiongozi mwandamizi nchini Tanzania katika serikali za
awamu nne zilizopita na amewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika
serikali zikiwemo ukuu wa mikoa ya Tanga na Singida, Katibu Mwenezi wa
Chama Cha Mapinduzi na Waziri katika wizara mbalimbali.
WALTER HAABARI inatoa pole kwa ndugu, jamaa na rafiki wa familia ya mzee Kingunge kwa msiba huu mzito wa Taifa.
Post a Comment
karibu kwa maoni