
Matokeo
ya awali ya uchaguzi wa ubunge Jimbo la Siha yameanza kubandikwa nje
ya vituo vya kupigia kura yakionyesha mgombea wa CCM, Dk Godwin Mollel
akiongoza kwa mbali katika baadhi ya vituo.
Katika
matokeo hayo, Dk Mollel anafuatiwa kwa mbali na mgombea wa Chadema,
Alvis Mossi huku wa CUF, Tumsifuel Mwanri akishika nafasi ya tatu
lakini kwa tofauti kubwa ya kura.
Baadhi
ya matokeo hayo ni kama ifuatavyo. Kituo cha Kirua–Kawate Kata ya
Siha, Wilaya ya Siha mgombea wa CCM alipata kura 208, huku Alvis wa
Chadema akipata kura 42 na Mwanri wa CUF akipata kura 10
Katika kituo cha Lawate namba 2 Kata ya Siha, CCM ilipata kura 300 na Chadema 21 huku CUF ikiambulia 0.
Kituo cha Lomakaa, CCM ilipata kura 190, Chadema 10 na CUF haikupata chochote.
Pia kituo cha Ofisi ya Kijiji Sanya Juu, CCM ilipata kura 284,Chadema 54 na CUF 1.
Kwa
upande wa kituo cha Sanya Juu, CCM ilipata kura 93,Chadema 50, CUF 0,
huku kituo cha Kaboko Kusini 2, CCM 403, Chadema 68 ,CUF na Sau zikiwa
hazijapata kitu.
Pia
Kituo kingine cha Kaboko B; CCM 106,CUF 76, Sau 0 na kituo cha Ofisi ya
VEO Merali Juu1; Chadema 33, CCM 64 huku CUF na Sau vikiwa havijapata
kitu. Ofisi ya VEO Merali Juu2: Chadema 22 na CCM 87.
Kituo
cha Pyarita kata ya Nasai Mgombea wa CCM alipata kura 194 huku Alvis
wa Chadema akipata kura 44 na Mwanri akipata Cuf akipata kura 5.
Post a Comment
karibu kwa maoni
EmoticonClick to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.