Akizungumza
na Walimu wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari zaidi ya 100 Wilaya ya
Kyela mkoa wa Mbeya Mwenyekiti wa Tume ya utumishi wa walimu Tanzania,
Bi. Oliver Muhaiki amesema mojawapo ya kazi kubwa ya tume hiyo ni
kusimamia maadili na wajibu wa walimu wanapokuwa wakitekeleza majukumu
yao.
Amesema baadhi ya walimu nchini wamekuwa wanashindwa kuzingatia maadili ya kazi yao ikiwa ni pamoja na kufanya mapenzi na wanafunzi na utoro kazini vitendo ambavyo amesema havipaswi kuvumiliwa na tume hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tume ya walimu Mektirisi Kapinga amesisitiza umuhimu wa walimu kufahamu Muundo wa tume hiya inapokuwa inasimamia masuala yanayowahusu walimu.
Aidha imebainishwa kwamba uwepo wa tume hiyo ambayo ni maalumu tu kwa walimu wa shule za msingi na sekondari za umma, kunawapa matumaini walimu wa Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya kutatuliwa changamoto zao.

Post a Comment
karibu kwa maoni