0
Image result for uwanja wa jamhuri dodoma 
Wakati ligi ya mkoa Dodoma ligi daraja la tatu  HATUA ya sita bora ikiendela kutimua vumbi katika uwanja wa Jamhuri  timu ya Area D kutoka K ndege hali yake sio nzuri kwani mpaka sasa hajaambulia pointi hata moja.
Timu ya jeshi la wananchi wa Tanzania  Gunners kutoka Ihumwa inafuatia ikiwa na alama 1.
Ajax ya Kondoa mpaka sasa imevuna alama 3,Watumishi kutoka Mpwapwa ina alama 4,Sheli ya Cmwino mjini ina alama 3,Gwasa ya Chang'ombe mjini inafikisha alama 6 baada ya kumfunga  Gunners 3-1.
Aidha Sheli imefikisha alama 6 baaada ya kumpiga Area d 5-0.
Ligi hiyo inatarajia kukamilika ijumaa ijayo  march 23.2018 ambapo msindi atapata nafasi ya kushiriki  ligi  daraja la pili.
 Mjumbe mwakilishi wa vilabu kutoka chma cha soka mkoani Dodoma [DUFA] Mweri Hamsini ambaye amekuwa akifuatilia michuano hiyo ameiambia WALTER HABARI kuwa ligi inaenda vizuri na hakuna figisu figisu zozote mpaka sasa,waamuzi wanatenda haki.
Viingilio katika ligi hiyo ni shilingi 1,000 kwa watu wote.
Wakati huo huo ligi daraja la tatu mkoa wa Manyara hatua ya sita bora  inatarajiwa kuanza kuchezwa wiki hii katika kituo cha Mbulu baada ya kuhamishwa kutoka Nangwa sababu ya uwanja kujaa Maji.
Katibu wa kamati ya mashindano wa chama cha soka mkoa wa Manyara(MARFA ) Yusuph Mdoe alisema hatua hiyo ya sita bora itachezwa kwa mtindo wa ligi yani kila timu itacheza na mwenzake ambapo timu itakayoongoza kwa pointi ndio itakuwa bingwa .
Alizitaja timu zilizotinga katika hatua hiyo kutoka kundi A kuwa ni  ni fire stone fc ya kiteto iliyokuwa na alama 9,Morning Star fc ya Mbulu yenye alama 9 pamoja na Babati Mashujaa (BM Sc ) ya Babati yenye alama 9 timu hizi zikitofautiana idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa.
 Kundi B zilizotinga sita  bora ni Usalama sc iliyoongoza kwa pointi 9 ikifuatiwa na Mrara fc yenye alama 9 timu zote za Babati zikiwa zimetofautiana mabao ya kufunga na kufungwa wakati nafasi ya tatu ni Halmashauri fc ya Hanang yenye alama 6.
Alizitaka timu hizo kujiandaa vyema ili kupata bingwa atakae kwenda kuiwakilisha Manyara vizuri kwenye Mashindano ya ligi ya mabingwa mikoa (RCL).
Alizitaja timu zilishuka daraja kuwa ni Magugu Rangers ya Babati,Gwadaat Fc, Nangwa, Green Star za Hanang pamoja na Red Star Fc ya Kiteto.
Michuano hiyo ilianza kutimua vumbi machi 5 mwaka huu kwa kuzishirikisha jumla ya timu 10 kutoka wilaya nne za Babati,Mbulu,Kiteto na Hanang katika makundi mawili ya A na B huku timu za  Simanjiro zikishindwa kushiriki kutokana na sababu ya ukata.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top