Waziri
Mkuu za zamani, Edward Lowassa amemueleza Rais mstaafu wa Awamu ya
Tatu, Benjamin Mkapa kwamba kauli yake aliyoitoa juzi akitaka kuwepo kwa
mjadala wa kitaifa kujadili hali ya elimu nchini ilikuwa ajenda yake
tangu alipokuwa CCM.
Lowassa
ametoa kauli hiyo jana Machi 19, 2018 katika taarifa yake kwa vyombo
vya habari iliyotolewa na msemaji wake, Aboubakar Liongo.
Katika
taarifa hiyo, Lowassa ambaye alijiunga Chadema mwaka 2015 baada ya jina
lake kukatwa katika mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM kusaka
mgombea wake wa urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015,
amesema suala la elimu pia lipo katika ilani ya uchaguzi ya Chadema.
Juzi
jioni katika hafla ya kumuaga Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma
(Udom), Profesa Idris Kikula, Mkapa alisema kuna janga katika elimu
nchini na kushauri kuitishwa kwa mdahalo wa wazi utakaoshirikisha
makundi yote ya jamii kwa ajili ya kujadili suala hilo.
Katika
taarifa yake hiyo, Lowassa amesema amesoma na kusikia taarifa ya Mkapa
akitaka kuwepo kwa mdahalo wa kitaifa kuhusu kushuka kwa elimu nchini.
“Nimefurahi
kuwa Mkapa ameliibua suala hili kwani hiyo ilikuwa ni ajenda yangu ya
kwanza tangu nikiwa ndani ya CCM na nje ya CCM. Pia Ilani ya uchaguzi ya
Chadema, elimu ndio ilikuwa ajenda kuu na tulisema tutaita mjadala wa
kitaifa kuhusu elimu na kuangalia wapi tumekwama na nini kifanyike,”
amesema Lowassa.
Lowassa
amedai ajenda hiyo sio ya CCM na hawataweza kuisimamia kwa sababu
wanataka kuendelea kutawala,ila hawataki Taifa lililoelimika vizuri na
linaloweza kuhoji.
Post a Comment
karibu kwa maoni