0

Timu ya Mpira wa miguu Mrara Fc yenye maskani yake mjini Babati mkoani Manyara imesema imesikitishwa sana na taarifa kuwa hawatoshiriki ligi kutokana na ukata unaoikabili timu hiyo.
Akizungumza na Walter Habari kocha wa kikosi hicho ameeleza kuwa taarifa hizo walizosikia kupitia redio Manyara FM kupitia kipindi cha Michezo kinachoendeshwa na mtangazaji John Walter kila siku saa 2:00 usiku,hazijawavunja moyo na kwamba wanaoeneza taarifa hizo hawaitakii mema timu hiyo.
Hata hivyo Mrara fc walipata udhamini kutoka chama cha soka wilaya ya Babati BDFA kwa mujibu wa Kocha wa Mrara Fc aliezungumza na WALTER HABARI baada ya mchezo wao wa ligi daraja la tatu mchezo walioshinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Halmashauri Fc ya Hanang.
Ligi hiyo daraja la tatu ngazi ya mkoa Manyara kwa mwaka huu inashirikisha timu kumi huku tatu zikishindwa kushiriki kutokana na ukata.
Aidha ratiba inaonyesha kuwa March 16 mzunguko wa kwanza unakamilika ambapo hatua ya robo fainali, nusu fainali na fainali itajulikana.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top