https://youtu.be/kSKZsexPfZ0
Baada ya vuta nikuvute ya ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa katika mkoa wa Manyara,hatimaye bingwa wa Mkoa amejulikana ni Usalama Sports Club.
Baada ya vuta nikuvute ya ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa katika mkoa wa Manyara,hatimaye bingwa wa Mkoa amejulikana ni Usalama Sports Club.
Akimtangaza bingwa wa mkoa katika ligi daraja la tatu
iliyomalizika mwanzoni mwa wiki hii katibu wa Mashindano Yusuph Mdoe amesema kuwa
baada ya Usalama kuandika barua na kuonekana wanacholalamikia kina mashiko
wamempa ubingwa.
Usalama waliandikia barua Kamati ya Mashindano inayosimamiwa
na chama cha soka mkoa MARFA kulalamika juu ya kitendo cha upangaji wa matokeo
kati mechi ya Firestone ya kiteto dhidi ya Morning Star ya Mbulu mchezo
uliomalizika kwa Firestone kushinda kwa idadi ya mabao mengi 8-2 Morning Star.
Mdoe ameeleza kuwa Usalama ametangazwa bingwa wa mkoa
Manyara baada ya mchezo wa Morning Star na Firestone kufutwa kwa kuonekana
kupangwa kwa matokeo kitendo ambacho ni kinyume na taratibu za mashindano.
Akizungumza na kipindi cha Sports Power kinachorushwa redio Manyara Fm Mlezi wa Usalama Sports Club
Mkuu wa upelelezi na Makosa ya jinai mkoa wa Manyara SSP Joshua Mwafulambo
amesema kwa sasa ni mwendo wa kusonga mbele huku akiwataka wadau wa Soka
kuisapoti timu kwa nguvu zote kwa kuwa ndio timu pekee ndani ya Manyara iliyopiga
hatua hadi daraja la pili[Kanda].
“Malengo ya Timu hii inayomilikiwa na wananchi kwa kushirikiana
na jeshi la polisi kupitia vikundi
shirikishi na polisi jamii, Mkoa wa Manyara ni kufika ligi kuu na kushuhudiwa
timu mbalimbali zikifika katika mkoa wetu kucheza soka.’alisema Mwafulambo.
Hata hivyo Morning Star na Firestone zote kwa pamoja
zimepigwa faini ya shilingi laki tano [500,000] na kufungiwa kujihusisha na
soka kwa miaka mitatu.
Mrara Fc pamoja na Bm Fc zenyewe zimekumbwa na adhabu ya
kufungiwa miaka mitatu baada ya kushindwa kuhudhuria uwanjani Mrara akishindwa kwenda uwanjani mchezo
miwili ,mmoja dhidi ya Bm Fc na mwingine dhidi ya Fire Stone bila kutoa taarifa
yeyote na Bm Fc alishindwa kuhudhuria katika mechi dhidi Fire Stone.
Post a Comment
karibu kwa maoni
EmoticonClick to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.