Baada
ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),
kuonyesha kuwa makusanyo ya serikali yanafikia lengo kwa takribani
asilimia 94, lakini fedha za maendeleo zinazotolewa ni takribani
asilimia 50 pekee Serikali imesema kwa mwezi inakusanya wastani wa Sh
trilioni 1.3, Sh bilioni 550 hulipa mishahara na Sh bilioni 600 hulipa
deni la taifa.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema hayo jana Alhamisi
Aprili 12, wakati akizungumza na waandishi wa habari kujibu sehemu ya
hoja zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu Hesabu za Serikali (CAG),
katika ripoti yake inayoishia Juni 2017 aliyoiwasilisha bungeni jana.
Dk.
Mpango alisema; “kwa hiyo maana yake kwenye Sh trilioni 1.3, umebakiwa
na bilioni 200 ambazo ndiyo hizo unatumia kuendesha Serikali, lakini
humo namo kuna shughuli nyingine ambazo hazikwepeki, kwa mfano askari
wetu shupavu wanalala nje lazima Serikali tuwape posho ya chakula, ndiyo
sisi tunaweza tukaendelea na vurugu huku bungeni tukabishana, tukala
nyumbani kwa amani.
“Kuna
mishahara ya Majaji lazima ilipwe na marupurupu yao mengine, kuna
viongozi wetu nao hawalali, niwahakikishie ni kawaida kabisa kumpigia
Rais simu saa nane, saa tisa yuko macho, hawa viongozi wamebeba dhamana
kubwa lazima Serikali iwahudumie.
“Kwa hiyo unaponiuliza hizi nyingine zinaenda wapi, naweza nikaendelea na kuendelea,” alisema Dk. Mpango.
Awali,
Dk. Mpango alisema Serikali ya awamu ya nne, ilikuwa inakusanya Sh
bilioni 850 kwa mwezi, lakini tangu Serikali ya awamu ya tano kuingia,
imekuwa ikikusanya wastani wa Sh trilioni 1.
“Kwa
hiyo ni ni rahisi sana kuhesabu hicho kinachoingia mfukoni, lakini ni
muhimu kuangalia sana hicho kinachotoka, zinatoka zinakwenda kwenye
nini.
“Ulipaji
wa deni la taifa inategemea, kwa mwezi inaweza ikatoka kati ya Sh
bilioni 600, tumewahi kwenda mpaka Sh bilioni 900, kutegemea na hayo
madeni yanaiva wakati gani, mwezi huu unaweza ukalipa Sh bilioni 600 na
kidogo, mwezi ujao ukalipa Sh bilioni 700, ni kwasababu ya tofauti ile
mikopo inaiva wakati gani.
“Ukichukua
wastani wa Sh bilioni 550 mishahara, ukaongeza Sh bilioni 600 kwaajili
ya kulipa deni, tayari Sh trilioni 1.1 umeitumia kwa hivyo vitu viwili
ambavyo huwezi kukwepa,” amesema Dk. Mpango.
Post a Comment
karibu kwa maoni