Usambazaji
wa gesi majumbani katika jiji la Dar es Salaam unaanza kesho Jumanne,
Aprili 24 huku bei ya gesi ikipungua kwa asilimia 40 ya bei ya sasa
kwenye mitungi.
Waziri
wa Nishati, Dk Medadi Kalemani ametoa kauli hiyo muda mfupi wakati
akijibu hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
katika utaratibu wa mawaziri waliojiwekea.
Dk
Kalemani amesema gharama za kuunganisha gesi kwa wateja watakaopitiwa
na bomba hilo itakuwa Sh 200,000 hadi 1 milioni kutegemeana na umbali
kutoka lilipo bomba kuu.
Ametaja
baadhi ya maeneo yatakayoanza kunufaika kuanzia kesho ni Ubungo,
Mwenge, Kijitonyama, Gongolamboto, Shekilango na Mikocheni na kazi hiyo
itadumu kwa miezi miwili.
Post a Comment
karibu kwa maoni