Rais
Yoweri Museveni amewaonya wananchi wa Uganda dhidi ya vitendo vya
kutumia mdomo katika kufanya mapenzi, akisema "mdomo uliumbwa kwa ajili
ya kula na si mapenzi".
Rais huyo wa muda mrefu nchini Uganda amesema utamaduni huo wa kutumia mdomo katika mapenzi uliletwa na wageni.
“Nichukue
nafasi hii kuonya watu wetu hadharani dhidi ya vitendo visivyo sahihi
vilivyoletwa na vinavyoendelezwa na wageni. Mojawapo ni mapenzi ya
kutumia mdomo. Mdomo ni kwa ajili ya kula si mapenzi.” Museveni alisema
hayo wiki iliyopita wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliorushwa
moja kwa moja na vituo vya televisheni.
Vyombo
vya habari vya Uganda vimeripoti onyo hilo na kuzua mijadala kwenye
mitandao ya kijamii, ambako baadhi ya watu wanapingana naye na wengine
kumpongeza.
Kauli
yake ilitoka siku chache baada ya kusambaa kwa picha zinazomuonyesha
ofisa mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Makerere akimnyonya sehemu za siri
mwanafunzi wake ofisini kwake.
Ofisa huyo, anayehusika na utawala, ameshasimamishwa kazi na analipwa nusu mshahara, wakati tukio hilo likichunguzwa.
Tukio hilo lilijulikana baada ya mwanafunzi huyo kusambaza picha alizojipiga wakati ofisa huyo akimfanyia kitendo hicho.
Mwanafunzi
huyo alisema ofisa huyo wa Makerere alimbusu sehemu zake za siri kwa
nguvu na alipiga picha hizo ili apate ushahidi kwa kuwa ofisi hiyo
haikuwa na kamera za usalama.
Post a Comment
karibu kwa maoni