Serikali imepanga kuajiri watumishi wa kada ya afya wapatao 25,000 katika mwaka wa fedha 2018/19.
Kauli
hiyo imetolewa bungeni mjini Dodoma leo Jumatatu Aprili 23, na Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), Josephat Kandege wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbulu
Mjini, Zacharia Issay (CCM).
Katika
swali la msingi Issay alitaka kujua serikali ina mkakati gani wa
kuongeza watumishi katika Hosptali ya Wilaya ya Mbulu ambapo Kandege
amesema tayari Tamisemi imeomba kibali cha kuajiri watumishi wa kada ya
afya 25,000 ili kuhakikisha kunakuwapo na watumishi wenye sifa stahiki
kwenye hospitali, vituo vyote vya afya na zahanati.
“Serikali
inaendelea na ujenzi wa vituo vya afya 208 nchi nzima ili kuboresha
huduna ya dharura kwa mama wajawazito, ujenzi wa vituo hivyo utagharimu
Sh bilioni 132.9 hadi kukamilika.
“Sambamba
na ujenzi huo, vituo hivyo vimetengewa Sh bilioni 35.7 kwa ajili ya
ununuzi wa vifaa na vifaa tiba ili kuviwezesha kutoa huduma kwa
wagonjwa,” amesema.
Post a Comment
karibu kwa maoni