Mwenyekiti
wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha amemaliza muda
wake wa majukumu ya tume hiyo kwa kipindi cha miaka mitano kilichoanzia
Aprili 30,2 013 hadi Aprili 29, 2018 ambapo yeye na wajumbe wa tume hiyo
wamekabidhi ripoti yao ya kazi.
Akitoa
taarifa yake kwa Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Jecha amesema
kuwa tume inaamini kwamba, mafanikio yaliyopatikana wakati wa
utekelezaji wa majukumu yake hasa ya kiuchaguzi yalitokana na
ushirikiano wa wadau mbalimbali na wananchi kwa jumla.
"Ndani
ya miaka mitano tume imeweza kuendesha jumla ya chaguzi ndogo nne,
zikiwemo chaguzi ndogo tatu za Udiwani na chaguzi moja ya uwakilishi
pamoja na kusimamia uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25,2015 na ule wa marudio
yake Machi 20, 2016. Tume imefanya mapitio ya majimbo ya uchaguzi na
kubadilisha mipaka ya majimbo ya uchaguzi, majina ya majimbo na kuongeza
idadi ya majimbo kutoka 50 hadi 54", ameeleza Jecha.
Pamoja
na hayo, Jecha ameendelea kwa kusema "Tume imeweza kufanya uandikishaji
wa wapiga kura kwa awamu mbili na kuliendeleza daftari la kudumu la
wapiga kura sambamba na kuendesha programu mbalimbali za elimu ya wapiga
kura kupitia vyombo vya habari, mikutano ya wadau, uchapishaji wa
vipeperushi, majarida na makala mbalimbali".
Aidha,
Mwenyekiti huyo amemueleza Dkt. Shein kuwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar
imechaguliwa kuwa kiongozi wa Uchaguzi Mkuu wa nchini Congo
utakaofanyika mwezi Disemba mwaka huu.
Kwa
upande wake, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein ameipongeza Tume
hiyo kwa kutekeleza vyema majukumu yake ndani ya miaka mitano kwa
kuendesha chaguzi zote .
"Tume
hii inastahiki pongezi kwa kuifanikisha vyema kazi waliyopewa ikiwa ni
pamoja na kuendesha chaguzi zote ukiwemo uchaguzi Mkuu, chaguzi ndogo na
ule uchaguzi wa marudio ambazo zote hizo zilifanywa kwa ufanisi
mkubwa", amesema Dkt. Shein.
Wajumbe
wa tume hiyo ambao wamemaliza muda wao ni Mwenyekiti mwenyewe Jecha
Salim Jecha, Jaji Abdul-hakim Ameir Issa, Balozi Omar Ramadhan Mapuri,
Nassor Khamis Mohammed, Ayoub Bakari Hamad, Haji Ramadhan Haji na Salmin
Senga Salmin ambao wote hao waliapishwa rasmi Mei,4, 2013.
Post a Comment
karibu kwa maoni