Aliye wahi kuwa Katibu
Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali wa Wizara ya Fedha na Mipango, katika Serikali
ya Awamu ya Nne, Bw. Ramadhani Musa Khijjah (65), amefariki dunia alfajiri ya
kuamkia leo katika eneo la Jet Lumo, wilayani Temeke, mkoani Dar es Salaam.
Marehemu amefariki akiwa nyumbani kwake, Jet Lumo, maeneo ya Yombo Malawi Hospital-Wilaya ya Temeke
Maziko yatafanyika
kesho April 18, katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, saa 10 jioni.
Msiba uko nyumbani kwa
marehemu Ramadhan Khijjah katika eneo la Jet Lumo, Yombo Malawi
Hospital-Temeke.
Marehemu Ramadhani
Khijjah aliteuliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
kuwa Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali wakati huo Wizara ikijulikana kama
Wizara ya Fedha na Uchumi, Novemba 23, mwaka 2008.
Alistaafu utumishi wa
umma mnamo na June 12, 2013 akiwa na umri wa miaka 60.
Wakati wa uhai wake, Marehemu
Khijjah, atakumbukwa kwa uchapakazi wake hodari, uadilifu, uzalendo na alichukia
vitendo vya rushwa,.
Imetolewa na
Benny Mwaipaja
Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na
Mipango
Post a Comment
karibu kwa maoni