0
Image result for katibu ccm manyara mwamlima
Katibu Wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Manyara Paza Mwamlima.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Babati vijijini Edna Edmund Khera amefariki dunia  baada ya kuanguka ghafla ofisini alipokuwa akiendelea na majukumu ya Chama.
Akithibitisha kutokea kwa Kifo hicho katibu wa ccm mkoa wa Manyara Paza Mwamlima amesema kuwa Edna amefariki ghafla leo saa tatu asubuhi akiwa ofisini.
Mwamlima amesema kuwa wameelezwa na Madaktari  kuwa kifo hicho kimesabishwa na presha kupanda juu na kupelekea mshipa kupasuka.
Mwili wake utaagwa kesho katika nyumbani kwake mjni Babati na  baadae kusafirishwa   kwenda wilaya ya  Mbinga mkoani Ruvuma kwa mazishi.

sikiliza hapa chini
https://youtu.be/9qLb3zzLUlw 

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top