Watu saba wamefariki dunia kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam.
Kamanda
wa polisi kanda maalum jiini Dar es salaam Lazaro Mambosasa
amethibitisha vifo hivyo, na kueleza kwamba mwili mmoja umekutwa ukielea
kuelekea maeneo ya Jangwani jijini Dar es salaam.
Sambamba
na hilo Kamanda Mambosasa amesema maeneo mengi jijini Dar es salaam
yamejaa maji, na kuwataka watu kuwa makini wanapotumia barabara hasa
sehemu zenye makorongo, na kuwaangalia zaidi watoto ambao wanapita mara
kwa mara wakienda shule au wakiwa wanarudi kutoka shule.
“Watu
wasijaribu maji, ukijaribu maji ujue utaondoka nayo, kwa hiyo watoto
wetu wanapokwenda shuleni tuwasindikize, sehemu nyingi zenye makorongo
kwa mfano kule Kinyerezi, kule Goba kule Makongo, zile shortcut zote
maji yamejaa, watu wajiepushe kutumia njia hizo, watapoteza watoto
wakiwa wanaenda au kutoka shule”, amesema Kamanda Mambosasa.
Jeshi
la Polisi limesema litaendelea kutoa taarifa za sehemu mbali mbali
kuhusu hali ya mvua, ambayo inaendelea kuathiri sehemu kubwa ya nchi.
Post a Comment
karibu kwa maoni