TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Zanzibar, Karume Boys imefungiwa mwaka mmoja kushiriki michuano ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Cup U17 na kupigwa faini ya dola za Kimarekani 15,000 kwa kosa la kupeleka wachezaji waliozidi umri.
Michuano ya CECAFA Challenge Cup U17 inaendelea nchini Burundi na Zanzibar inadaiwa kuorodhesha wachezaji waliozaliwa kabla ya Januari 1 mwaka 2002, ambao wazi wamezidi umri unaotakiwa wa miaka 17.
Jana timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Tanzania Bara, Serengeti Boys ilitoa sare ya 1-1na Uganda katika mechi yake kwanza ya michuano hiyo.
Karume Boys
Ilisafiri kwenda Burundi April 12 na kupewa baraka zote na
Naibu Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Lulu Msham ikiwa na Jumla ya msafara wa watu 29 wakiwemo Wachezaji 23, Makocha 2 na
Viongozi 4 wameondoka Zanzibar kwa Ndege kwenda Burundi katika Mashindano
hayo yaliyoanza kuanza kutimua vumbi lake April 14 na yanatarajiwa kukamilika April 28, 2018 ambapo
Zanzibar ilipangwa kundi ‘B’ pamoja na ndugu zao Tanzania bara, Sudan na Uganda
huku kampeni zake Zanzibar kuwania kombe hilo zilitarajiwa kuanza jana April 15 kwa kucheza na
Sudan katika uwanja wa Gitega majira ya saa 7:30 za mchana kabla ya kukutwa na mkasa huo.
Walter Habari inatoa pole kwa Wazanzibar ila Vongozi wajitahmini kwa kilichotokea.
Post a Comment
karibu kwa maoni