Rais
Dkt Magufuli ameyasema hayo leo, katika hotuba yake aliyoitoa wakati wa
maadhimisho ya sherehe za miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na
Zanzibar.
“Nilifanikiwa
kuiona Dodoma ilivyokuwa. Imejengwa kila mahali, na Dodoma kweli ni
Makao Makuu. Tulizoea Dar es Salam ndiyo yalikuwa makao makuu kwa wakati
ule, na paliitwa Jiji.Nikaona niangalie katika nchi yetu tuna
Halmashauri ngapi, tuna manispaa ngapi na mimi nina mamlaka gani katika
kutengeneza majiji au manispaa au kadhalika,” amesema Rais Magufuli.
“Nikakuta
Arusha ni jiji, Tanga ni jiji, nikaambiwa Dodoma ni Manispaa, nikasema
haiwezekani. Kwahivyo kuanzia leo Dodoma linakuwa Jiji,” amesema Rais
Magufuli.
Vile
vile Rais MAgufuli amempandisha hadhi Mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma
kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kutokana na kupanda hadhi yake.
Post a Comment
karibu kwa maoni