Akizungumza
bungeni leo Aprili 17, Waziri Mwakyembe amesema serikali imeshatunga
sheria inayowabana wasanii na kudhibiti maudhui yasiyo na maadili
mitandaoni.
Mbali
na hilo Mwakyembe ameagiza msanii mwingine Nandi kusakwa na polisi
akisisitiza kauli yake kuwa Tanzania siyo kokoro la uchafu.
Ametoa
kauli hiyo wakati anajibu swali la nyongeza la mbunge wa Ulanga Godluck
Mlinga aliyetaka kujua serikali ina mkakati gani kukomesha tabia za
baadhi ya watu wanaotumia mitandao vibaya ikiwemo kuhamasisha masuala ya
ushoga.
Awali
serikali ilitaja changamoto kubwa inayolikabili taifa ni athari ya
utamaduni wa nje katika maadili, mila na desturi za Mtanzania kutokana
na kuwepo na muingiliano mkubwa wa watu duniani.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Juliana
Shonza wakati akijibu swali la mbunge, Nuru Awadh Bafadhili.
Mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mkakati gani madhubuti wa kuhakikisha vijana wa Kitanzania wanasimamia maadili.
Hata
hivyo Shonza amesema kinacholeta shida hadi nyimbo kuwa hazina maadili
ni tabia ya wasanii kutopeleka nyimbo zao kuhaririwa katika baraza la
Sanaa la Taifa (BASATA)
Post a Comment
karibu kwa maoni