Spika
wa Bunge, Job Ndugai ametoa sababu za kiongozi wa upinzani bungeni
kutokuwa na gari lake linalohudumiwa na Bunge kuwa ni kutokana na dereva
wake kustaafu.
Spika
Ndugai amesema dereva wa gari hilo alistaafu katika kipindi cha Bunge
la Tisa lakini aliendelea kuwa na mkataba kwa vipindi vyote hivyo sasa
Bunge limeona umri wake umekuwa mkubwa zaidi.
Ndugai
ametoa kauli hiyo leo Jumanne, Aprili 17 wakati anatolewa ufafanuzi wa
mwongozo ulioombwa April 12 na Mbunge Ukonga(Chadema), Mwita Waitara
kuhusu watumishi wa upinzani walioondolewa.
Spika
Ndugai amekiri kuwa hawapo baada ya kumaliza muda wao wa mkataba tangu
Desemba mwaka jana na akasema kwa sasa wanaendelea kutazama na
watalizungumza kwani linahitaji mjadala mpana hivyo akaomba upinzani
wasigomee kusoma hotuba za upinzani.
Kiongozi
huyo amesema mbali na watumishi wanne wa upinzani, lakini Bunge
limewafungashia virago watumishi watano wa upande wa CCM hivyo nao
hawana watendaji hadi Bunge litakapoamua vinginevyo kutokana na mambo ya
kiusalama.
Post a Comment
karibu kwa maoni